Wilaya ya Bunda mkoani Mara nchini Tanzania wamefikiwa na habari njema za Yesu Kristu aliye hai. Wainjilisti walipita mitaani kuhubiri habari njema za Ufalme wa Mbinguni na wengi kuamua kumpa Yesu Kristo maisha yao kupitia vitabu vya wokovu vinavyogaiwa bure vikiwa na maombi ya Toba ndani yake na mwongozo wa Neno la Mungu kwa kondoo wapya wanaoanza safari mpya ya wokovu. Ni wakati wa kubadili maisha yetu na kuamua kuishi maisha safi yanayompendeza Mungu; Luka 10:2 ” Akawaambia,Mavuno ni mengi,lakini wavunaji ni wachache,Kwa hivyo,mwombeni mwenye shamba atume wavunaji shambani mwake”. Haya ni maneno Bwana Yesu aliwaambia watumishi wake nasi tunapaswa kuhubiri habari njema za Ufalme wa Mbinguni na kuwaleta wengi kwa Bwana wetu na mwokozi wetu Yesu Kristo aliye hai.