VITABU VYA WOKOVU MKOANI TABORA-TANZANIA

Basi, enendenimkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote,(Mathayo 28:19-20).

Haya ni Maneno Bwana wetu na Mwokozi wetu Yesu Kristo aliye hai ametuamuru watenda kazi wake kumkusanyia mavuno yake,kuwaleta wengi kwake na kuuingia Ufalme wake wa Mbinguni kabla ya Parapanda.

Ugawaji wa vitabu vya wokovu Singida – Tanzania

Mkoa wa Singida nchini Tanzania wamefikiwa na habari njema za Yesu Kristu aliye hai. Katika Semina ya Neno la Mungu,walifanikiwa fikiwa na Neema hii ya Neno la Mungu kwa njia ya vitabu ili waendelee kujifunza Neno la Mungu na kuukulia wokovu.Ni wakati wa kubadili maisha yetu na kuamua kuishi maisha Matakatifu na safi yanayompendeza Mungu; Luka 10:2 ” Akawaambia,Mavuno ni mengi,lakini wavunaji ni wachache,Kwa hivyo,mwombeni mwenye shamba atume wavunaji shambani mwake”. Haya ni maneno Bwana Yesu aliwaambia watumishi wake nasi tunapaswa kuhubiri habari njema za Ufalme wa Mbinguni na kuwaleta wengi kwa Bwana wetu na mwokozi wetu Yesu Kristo aliye hai.

Ripoti Kitabu Maombi 16 Mkoani Tabora – Tanzania.

Kitabu Maombi 16 jinsi ya kuomba maombi mbalimbali na kujibiwa na Mungu kimekuwa msaada mkubwa kwa wakristo wengi.Kimekuwa msaada katika kumwongoza Mkristo jinsi ya kuomba,kujisimamia na Neno la Mungu katika maombi ya kile siku na hata katika kujiombea mwenyewe pale unapohitaji msada wa Kiroho zaidi. Mpendwa/Mkristo akimshukuru Bwana kwa msaada mkubwa alioupata kupitia kitabu hichi lakini pia jinsi kilivyomsaidia kumwona Mungu zaidi na maisha yake kubadilika pia. Mbali na mwongozo wa kiroho kitabu hichi kimesaidia wengi kupokea uponyaji kwa magonjwa na vifungo mbalimbali walivyofungwa na adui kupitia maombi mbalimbali yaliyomo ndani ya kitabu. Tunamshukuru Bwana Yesu aliye hai kwa kuzidi fungua wengi na kuwaleta wengi katika Ufalme wake wa Mbinguni amina.