Mkoa wa Singida nchini Tanzania wamefikiwa na habari njema za Yesu Kristu aliye hai. Katika Semina ya Neno la Mungu,walifanikiwa fikiwa na Neema hii ya Neno la Mungu kwa njia ya vitabu ili waendelee kujifunza Neno la Mungu na kuukulia wokovu.Ni wakati wa kubadili maisha yetu na kuamua kuishi maisha Matakatifu na safi yanayompendeza Mungu; Luka 10:2 ” Akawaambia,Mavuno ni mengi,lakini wavunaji ni wachache,Kwa hivyo,mwombeni mwenye shamba atume wavunaji shambani mwake”. Haya ni maneno Bwana Yesu aliwaambia watumishi wake nasi tunapaswa kuhubiri habari njema za Ufalme wa Mbinguni na kuwaleta wengi kwa Bwana wetu na mwokozi wetu Yesu Kristo aliye hai.