Ugawaji Vitabu vya wokovu Makambako – Tanzania.

Ni wakati habari njema za Ufalme wa Mbinguni za Yesu Kristo aliye hai,zikiendelea fikia wengi na wokovu ukipokelewa na wengi na kuuingia Ufalme wa Mbinguni. Kituo cha Treni wilaya ya Makambako walifikiwa na Neema hii ya kufikiwa na wokovu kupitia vitabu hivi ya Mpokee Yesu uuingie Ufalme wa Mbinguni. Mpe Yesu maisha yako sasa,hukumu ya mwisho imekaribia,Yesu anakupenda, acha maisha ya dhambi ichague Nuru sasa/chagua wokovu.

Ugawaji wa Vitabu vya wokovu Bunda -Tanzania

Wilaya ya Bunda mkoani Mara nchini Tanzania wamefikiwa na habari njema za Yesu Kristu aliye hai. Wainjilisti walipita mitaani kuhubiri habari njema za Ufalme wa Mbinguni na wengi kuamua kumpa Yesu Kristo maisha yao kupitia vitabu vya wokovu vinavyogaiwa bure vikiwa na maombi ya Toba ndani yake na mwongozo wa Neno la Mungu kwa kondoo wapya wanaoanza safari mpya ya wokovu. Ni wakati wa kubadili maisha yetu na kuamua kuishi maisha safi yanayompendeza Mungu; Luka 10:2 ” Akawaambia,Mavuno ni mengi,lakini wavunaji ni wachache,Kwa hivyo,mwombeni mwenye shamba atume wavunaji shambani mwake”. Haya ni maneno Bwana Yesu aliwaambia watumishi wake nasi tunapaswa kuhubiri habari njema za Ufalme wa Mbinguni na kuwaleta wengi kwa Bwana wetu na mwokozi wetu Yesu Kristo aliye hai.

Ugawaji wa vitabu vya wokovu Tabora- Tanzania

Ni wakati sasa wa wengi kumrudia Bwana na kuuingia Ufalme wake wa Mbinguni kabla haujaondolewa. Kupitia kitabu cha Mpokee Yesu uuingie Ufalme wa Mbinguni vinavyogaiwa bure kuwa msaada mkubwa wengi kumpa Yesu Kristo aliye hai maisha yao na kuuchagua Ufalme wake wa Nuru/wa Mbinguni sawasawa na Neno lake; Luka 10:2 ” Akawaambia,Mavuno ni mengi,lakini wavunaji ni wachache,Kwa hivyo,mwombeni mwenye shamba atume wavunaji shambani mwake”. Hivyo wilaya ya Nzega -Tabora nao wamefikiwa na wokovu na habari njema za Ufalme wa Mbinguni.